RORYA-MPYA
"Tunaunganisha Wana-Rorya Wote Popote Walipo kwani Maendeleo ya Rorya ni Umoja Wetu"
Wednesday, 30 March 2016
Saturday, 26 March 2016
SABABU ZA KUWEKEZA KATIKA WILAYA YA RORYA
SABABU ZA KUWEKEZA KATIKA WILAYA YA RORYA
Kuna sababu kadha wa kadha wa
kuwekeza katika wilaya ya Rorya. Licha ya faida utakayoweza kutengeneza vile
vile kuna mazingira mazuri kwa ukuaji wa biashara yako. Baadhi yao ni pamoja
na;
1.
Hali
ya hewa tulivu kwa kilimo na ufugaji 2. Uwepo wa ziwa victoria katika ukanda huu inatoa fursa ya uwekezaji kwenye uvuvi, viwanda vikuwa na vidogo, kilimo cha umwagiliaji na kadhalika.
3. Uwepo wa ardhi ya kutosha kwa uwekezaji wa kilimo, biashara pamoja na miradi mingine mikubwa na midogo.
4. Uwepo wa amani na utulivu itakayopelekea ustawi wa biashara yako
5. Upatikanaji wa nguvu kazi ya kutosha.
6. Wilaya ya rorya ina miundombinu kama vile barabara inayounganisha wilaya ya karibu kama vile Tarime na Musoma. Vile vile wilaya ya Rorya ipo karibu nan nchi ya jirani na Kenya hii itakusaidia kupanua wigo wa soko la bidhaa zako.
7. Ukarimu wa watu, wakazi wa wilaya ya Rorya ni wakarimu na wanapenda wageni pia
HALI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA
MBALIMBALI KATIKA WILAYA YA RORYA
Hali ya Uwekezaji katika Kilimo
Katia ya wilaya 6 za mkoa wa mara
(Rorya, Serengeti, Tarime, Musoma, Butiama na Bunda), ni wilaya mbili pekee,
Rorya na Bunda imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara uwepo wa njaa na ukosefu wa chakula cha
kutosha. Hali hii inapelekewa na uzalishaji mdogo katika sekta ya kilimo katika
hizi wilaya mbili ukilinganisha na wilaya nyingine. Uzalishaji mdogo imekuwa
ikihusishwa na vitu vifuatavyo;
Kwanza eneo la wilaya ya hii ina ukubwa wa heraki 291,375
inayofaa kwa kilimo lakini ni hekari 130,481
pekee ndio inayolimwa mpaka sasa. Vilevile eneo lenye ukubwa wa kilometa za
mraba takriban 17,350 inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ni kilometa za
mraba 1,039 pekee ndio kilimo cha umwagiliaji inafanyika. Pili, Kilimo katika
wilaya ya Rorya kwa kiasi kikubwa inategemea jembe la mkono pamoja na ya
kukokota na Ng’ombe. Hii hupelekea shuguli ya kilimo kuwa na tija ndogo. Aidha
kilimo cha kisasa kinafanyika lakini kinafanywa na watu wachache.
Fursa za uwekezaji katika kilimo
Viwanda vya kuchakata na Kusindika mazao ya Kilimo: Ukiachilia mbali uwepo wa mazingira mazuri ya Uwekezaji
katika uchakataji na usindikaji wa mazao ya chakula na biashara, wilaya
imepakana na wilaya za jirani itakayokuwezesha kujihakikishia soko na
upatikanaji wa Mazao ghafi.
Kilimo cha Umwagiliaji: Wilaya ya Rorya ina Vyanzo vikubwa vya maji ikiwemo Ziwa
Viktoria, Mto Mara, Mto Mori na Mto Bukwe achilia mbali mito mingine midogo
midogi isiyokauka mwaka mzima. Kwa mfano katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya
Mara (Chereche, Ochuna) hutumia maji ya Mto Mara na Mto Mori kwenye Kilimo cha
Mpunga. Uwekezaji katika sekta hii inaweza kufanyika kwenye Viwanda na mashine
za kukoboa mpunga, ujenzi wa Magodauni na ujenzi wa mabwawa ya Umwagiliaji.
Hali ya uwekezaji katika Mifugo
Inakadiriwa kuwa 51% ya kaya zote katika mkoa wamara
zinazojihusisha na Kilimo wanafuga pia. Mkoa wa Mara mwaka 2011/12 ilikuwa na
jumla ya mifugo (ng’ombe, mbuzi, Kondoo na punda) 2,222,542 ambapo 1187003 (ng’ombe), 662,444 (Mbuzi),
262,627 (kondoo) na 15,086 (punda). Jedwali ifuatayo inaonyesha Mgawanyo wa
Idadi ya Mifugo katika kila wilaya. (Wilaya ya Rorya imewekeza kivuli).
Makadirio ya Mifugo Mkoa wa Mara mwaka 2011/12
Wilaya
|
Ng'ombe
|
Mbuzi
|
Kondoo
|
Punda
|
Butiama
|
300,023
|
141,245
|
35,096
|
2,920
|
Bunda
|
331283
|
97,948
|
52,455
|
950
|
Tarime
|
148,278
|
173,746
|
34,558
|
9,745
|
Serengeti
|
345647
|
151928
|
99035
|
638
|
Rorya
|
157,064
|
97,577
|
41,483
|
833
|
1,282,295
|
662,444
|
262,627
|
15,086
|
Chanzo:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Musoma, 2012
Huduma ya Matibabu ya Mifugo (Veterinary Service): Licha ya uwepo wa mifugo mingi katika Mkoa wa Mara
hususani katika wilaya ya Rorya bado hakuna wataalam wa kutosh, waliosomea na
waliobobea katika magonjwa na maradhi mbalimbali yanayoksumba mifugo. Bado
inahitajika uwekezaji mkubwa katika fani hii.
Ranchi: Bado kuna maeneo makubwa katika Wilaya ya Rorya inayofaa kuanzisha Ranch
kubwa za mifugo hususani Ng’ombe. Vilevile kuna hali ya hewa wezeshi kwa ajili
ya uwekezaji huu. Uwekezaji kwenye Ranch sio tu itaongeza ubora bidhaa
zitokanazo na mifugo lakini pia itawezesha wazawa kujifunza mbinu za kisasa za
ufugaji.
Viwanda vya bidhaa zitokanazo na maziwa (Dairy
Industries):
Soko la bidhaa zitokanazo na Maziwa kama vile maziwa
yenyewe, Siagi, Mtindi, cheese na kadhalika inazidi kushika kasi ndani na nnje
ya nnchi. Uzalishaji wa sasa haitoshi kukidhi mahitaji, hivyo basi uwekezaji
kwenye Fursa hii inaweza kupelekea faida kubwa sana kwa muwekezaji na jamii
kiujumla.
Viwanda vya kudindika nyama: Bado hakuna viwanda vya kutosha katika mkoa mzima wa Mara
licha ya uwepo wa Mifugo mingi hususan Ng’ombe. Uwekezaji huu inaweza kufanyika
kwanza kwa kuanzisha machinjio bora na ya kisasa pamoja na viwanda vya
kusindika nyama na kupata bidhaa kama vile nyama yenyewe, soseji na nyama ya
kwenye pakti. Uanzishwaji wa viwanda kama hivi vitapelekea uongezaji wa thamani
ya bidhaa za wakulima. Viwanda kama hivi vimeshaanzishwa katika wilaya za
jirani kama vile Musoma na Serengeti.
![](file:///C:\Users\okanda\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.png)
Hali ya Uwekezaji katika Viwanda
Uwekezaji katika sekta ya viwanda katika wilaya ya Rorya
na Mkoawa Mara kiujumla bado iko chini. Mkoa mzima wa Mara in Viwanda 18 pekee
ikiwemo vidogo, vya kati na Vikubwa. Miongoni mwa viwanda 18 Wilaya ya Rorya in
Viwanda vinne (4) pekee. Jedwali ifuatayo inaonesha viwanda vilivyopo ndani ya
mkoa wa Mara. (Wilaya ya Rorya imewekewa Kivuli).
Hali ya Uwekezaji Kwenye Viwanda Katika Mkoa Wa Mara
S/N
|
Wilaya
|
Jina la Kiwanda
|
Bidhaa inayozalishwa
|
Uzalishaji Mwaka 2011/12
|
Soko la Bidhaa
|
1
|
Bunda
|
Orlam(t) ltd
|
Uchakataji Pamba
|
Kilogramu 8.5 milioni
|
Nnje ya nchi
|
Bundaa oil industry
|
Mafuta ya Kupikia
|
Lita 2.7 million
|
Nnje ya nchi
|
||
S&C Ginning Co. Ltd.
|
Uchakataji Pamba
|
Kilogramu 8 million
|
Nnje ya nchi
|
||
Mafuta ya Kupikia
|
Lita 1.8 millioni
|
Ndani ya nchi
|
|||
2
|
Tarime
|
Mara Coffee Ltd.
|
Kahawa Safi
|
Tani 942.3
|
Moshi na Soko la Kimataifa
|
Amir Hamza (T) Ltd
|
Kahawa Safi
|
Tani 77.6
|
Moshi na Soko la Kimataifa
|
||
ESSAB (T)
|
Kahawa Safi
|
Tani 174.8
|
Moshi na Soko la Kimataifa
|
||
3
|
Serengeti
|
Viwanda viwili (2) vya kutengeneza mafuta ya kupikia ya
alizeti
|
Mafuta ya kupikia
|
Kiwanda kimoja kimefungwa na kingine hakijaanza kufanya
kazi
|
Ndani ya nchi
|
4
|
Musoma
|
Prime Catch
|
Minofu ya Samaki
|
Kilogramu 20,200,451
|
Ulaya na
Kenya
|
Musoma processing
|
Minofu ya Samaki
|
Kilogramu 19,201,500
|
Ulaya na
Kenya
|
||
New Musoma textile
|
Nguo
|
Mita 102,120,201
|
Ndani ya nchi
|
||
Musoma Dairy
Processing Co
|
Maziwa
|
Lita 150,000
|
Kenya na
Musoma
|
||
Victoria milk
|
Maziwa
|
Lita 369,118
|
Mara
|
||
Winners co. ltd
|
Mikate
|
Pisi 1,220,101
|
Mara
|
||
Keki
|
Pisi 2,901,215
|
Bunda
|
|||
Skonzi
|
Pisi 1,119,010
|
Mwanza
|
|||
5
|
Rorya
|
Baraki Sisters Milk
|
Milk
|
-
|
Rorya,shirati na
Musoma
|
Riagoro
|
Soap
|
-
|
Rorya
|
||
Utegi
|
Animal skin
|
-
|
Rorya
|
||
Utegi
|
Spices
|
-
|
Ndani ya Nchi
|
Chanzo: Mara Region Investment Profile 2012
Hali ya uwekezaji katika Uchimbaji Madini
Madini ni miongoni mwa rasilimali zinazopatikana katika
wilaya Rorya. Japokuwa bado hakuna Takwimu juu ya hali ya uchimbaji katika
wilaya ya Rorya lakini kuna viashiria mbalimbali vya uwepo wa madini katika
baadhi ya maeneo ya wilaya hii. Aidha kwa uopande mwingine utafiti wa awali
inaonesha kwamba Gesi imeshagundulika katika maeneo ya Kogaja na Nyamusi.
Kutokana na ugunduzi huu inahitajika
uwekezaji katika sekta mbalimbali za kijamii itakayoenda sambamba na ukuaji wa
sekta ya madini. Kwa mfano Sekta ya madini inaenda sambamba na uboreshaji wa
huduma za usafiri, mawasiliano, migahawa na mahoteli. Kwahiyo hizi zote ni
fursa inayohitaji uwekezaji tena wa haraka. Vilevile inahitajika makampuni
yatakayowekeza katika uchimbaji mkubwa na yenye tija.
Hali ya uwekezaji katika Mali asili na
Utalii
Sekta ya utalii ni moja ya sekta zinazopaisha mkoa wa
Mara. Baadhi ya vivutio vikubwa vinavyopatikana katika Mkoa wa Mara ni pamoja
na Mbuga maarufu ya Serengeti pamoja na Ghuba ya Speke (Wilaya ya Bunda). Hizi
zote zinatoa fursa ya ujenzi wa mahoteli ya kitalii na biashara mbalimbali
inayoendana na Sekta husika. Katika wilaya ya Rorya vitvutio vya utalii ni visiwa
vya Ryamakabe na Bugambwa. Haya maeneo yanahitajika uwekezaji wa makampuni ya
utalii na miundombinu za kitalii ikiwemo mahoteli, maduka na biashara zingine
zinazoendana na utalii.
Subscribe to:
Posts (Atom)