Saturday, 26 March 2016

SABABU ZA KUWEKEZA KATIKA WILAYA YA RORYA



SABABU ZA KUWEKEZA KATIKA WILAYA YA RORYA
Kuna sababu kadha wa kadha wa kuwekeza katika wilaya ya Rorya. Licha ya faida utakayoweza kutengeneza vile vile kuna mazingira mazuri kwa ukuaji wa biashara yako. Baadhi yao ni pamoja na;
1.   Hali ya hewa tulivu kwa kilimo na ufugaji 
2.   Uwepo wa ziwa victoria katika ukanda huu inatoa fursa ya uwekezaji kwenye uvuvi, viwanda vikuwa na vidogo, kilimo cha umwagiliaji na kadhalika. 
3.   Uwepo wa ardhi ya kutosha kwa uwekezaji wa kilimo, biashara pamoja na miradi mingine mikubwa na midogo. 
4.   Uwepo wa amani na utulivu itakayopelekea ustawi wa biashara yako 
5.   Upatikanaji wa nguvu kazi ya kutosha. 
6.   Wilaya ya rorya ina miundombinu kama vile barabara inayounganisha wilaya ya karibu kama vile Tarime na Musoma. Vile vile wilaya ya Rorya ipo karibu nan nchi ya jirani na Kenya hii itakusaidia kupanua wigo wa soko la bidhaa zako. 
7.   Ukarimu wa watu, wakazi wa wilaya ya Rorya ni wakarimu na wanapenda wageni pia

HALI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA MBALIMBALI KATIKA WILAYA YA RORYA
 Hali ya Uwekezaji katika  Kilimo
Takriban 90% ya wakazi wa Mkoa wa Mara ikiwemo Wilaya ya Rorya hutegemea kilimo kama njia ya kujikwamua kimaisha na Kiuchumi (Mara Region Investment Profile, 2012). Kilimo huchangia 60% ya pato la ndani ya mkoa. Mazao yanayolimwa nipamoja na Mihogo, mahindi, Mtama, Uwele, mpunga, maharage na Viazi vitamu. Pamba ni zao kuu la bashara inayolimwa karibia Wilaya zote mkoani Mara ikiwemo wilaya ya Rorya. Mazao mengine ya biashara yanayolimwa katika wilaya ya Rorya (kwa kiasi kidogo) ni pamoja na Alizeti na karanga.

Katia ya wilaya 6 za mkoa wa mara (Rorya, Serengeti, Tarime, Musoma, Butiama na Bunda), ni wilaya mbili pekee, Rorya na Bunda imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara  uwepo wa njaa na ukosefu wa chakula cha kutosha. Hali hii inapelekewa na uzalishaji mdogo katika sekta ya kilimo katika hizi wilaya mbili ukilinganisha na wilaya nyingine. Uzalishaji mdogo imekuwa ikihusishwa na vitu vifuatavyo;

Kwanza eneo la wilaya ya hii ina ukubwa wa heraki 291,375 inayofaa kwa kilimo lakini ni hekari  130,481 pekee ndio inayolimwa mpaka sasa. Vilevile eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba takriban 17,350 inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ni kilometa za mraba 1,039 pekee ndio kilimo cha umwagiliaji inafanyika. Pili, Kilimo katika wilaya ya Rorya kwa kiasi kikubwa inategemea jembe la mkono pamoja na ya kukokota na Ng’ombe. Hii hupelekea shuguli ya kilimo kuwa na tija ndogo. Aidha kilimo cha kisasa kinafanyika lakini kinafanywa na watu wachache.

Fursa za uwekezaji katika kilimo

Viwanda vya kuchakata na Kusindika mazao ya Kilimo: Ukiachilia mbali uwepo wa mazingira mazuri ya Uwekezaji katika uchakataji na usindikaji wa mazao ya chakula na biashara, wilaya imepakana na wilaya za jirani itakayokuwezesha kujihakikishia soko na upatikanaji wa Mazao ghafi.

Kilimo cha Umwagiliaji: Wilaya ya Rorya ina Vyanzo vikubwa vya maji ikiwemo Ziwa Viktoria, Mto Mara, Mto Mori na Mto Bukwe achilia mbali mito mingine midogo midogi isiyokauka mwaka mzima. Kwa mfano katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Mara (Chereche, Ochuna) hutumia maji ya Mto Mara na Mto Mori kwenye Kilimo cha Mpunga. Uwekezaji katika sekta hii inaweza kufanyika kwenye Viwanda na mashine za kukoboa mpunga, ujenzi wa Magodauni na ujenzi wa mabwawa ya Umwagiliaji.

Hali ya uwekezaji katika Mifugo
Inakadiriwa kuwa 51% ya kaya zote katika mkoa wamara zinazojihusisha na Kilimo wanafuga pia. Mkoa wa Mara mwaka 2011/12 ilikuwa na jumla ya mifugo (ng’ombe, mbuzi, Kondoo na punda)  2,222,542 ambapo 1187003 (ng’ombe), 662,444 (Mbuzi), 262,627 (kondoo) na 15,086 (punda). Jedwali ifuatayo inaonyesha Mgawanyo wa Idadi ya Mifugo katika kila wilaya. (Wilaya ya Rorya imewekeza kivuli).

Makadirio ya Mifugo Mkoa wa Mara mwaka 2011/12
Wilaya
Ng'ombe
Mbuzi
Kondoo
Punda
Butiama
300,023
141,245
35,096
2,920
Bunda
331283
97,948
52,455
950
Tarime
148,278
173,746
34,558
9,745
Serengeti
345647
151928
99035
638
Rorya
157,064
97,577
41,483
833

1,282,295
662,444
262,627
15,086
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Musoma, 2012


Huduma ya Matibabu ya Mifugo (Veterinary Service): Licha ya uwepo wa mifugo mingi katika Mkoa wa Mara hususani katika wilaya ya Rorya bado hakuna wataalam wa kutosh, waliosomea na waliobobea katika magonjwa na maradhi mbalimbali yanayoksumba mifugo. Bado inahitajika uwekezaji mkubwa katika fani hii.
Ranchi: Bado kuna maeneo makubwa katika Wilaya ya Rorya inayofaa kuanzisha Ranch kubwa za mifugo hususani Ng’ombe. Vilevile kuna hali ya hewa wezeshi kwa ajili ya uwekezaji huu. Uwekezaji kwenye Ranch sio tu itaongeza ubora bidhaa zitokanazo na mifugo lakini pia itawezesha wazawa kujifunza mbinu za kisasa za ufugaji.

Viwanda vya bidhaa zitokanazo na maziwa (Dairy Industries):
Soko la bidhaa zitokanazo na Maziwa kama vile maziwa yenyewe, Siagi, Mtindi, cheese na kadhalika inazidi kushika kasi ndani na nnje ya nnchi. Uzalishaji wa sasa haitoshi kukidhi mahitaji, hivyo basi uwekezaji kwenye Fursa hii inaweza kupelekea faida kubwa sana kwa muwekezaji na jamii kiujumla.

Viwanda vya kudindika nyama: Bado hakuna viwanda vya kutosha katika mkoa mzima wa Mara licha ya uwepo wa Mifugo mingi hususan Ng’ombe. Uwekezaji huu inaweza kufanyika kwanza kwa kuanzisha machinjio bora na ya kisasa pamoja na viwanda vya kusindika nyama na kupata bidhaa kama vile nyama yenyewe, soseji na nyama ya kwenye pakti. Uanzishwaji wa viwanda kama hivi vitapelekea uongezaji wa thamani ya bidhaa za wakulima. Viwanda kama hivi vimeshaanzishwa katika wilaya za jirani kama vile Musoma na Serengeti.
Hali ya Uwekezaji katika Viwanda
Uwekezaji katika sekta ya viwanda katika wilaya ya Rorya na Mkoawa Mara kiujumla bado iko chini. Mkoa mzima wa Mara in Viwanda 18 pekee ikiwemo vidogo, vya kati na Vikubwa. Miongoni mwa viwanda 18 Wilaya ya Rorya in Viwanda vinne (4) pekee. Jedwali ifuatayo inaonesha viwanda vilivyopo ndani ya mkoa wa Mara. (Wilaya ya Rorya imewekewa Kivuli).

 Hali ya Uwekezaji Kwenye Viwanda Katika Mkoa Wa Mara
S/N
Wilaya
Jina la Kiwanda
Bidhaa inayozalishwa
Uzalishaji Mwaka 2011/12
Soko la Bidhaa
1
Bunda
Orlam(t) ltd
Uchakataji Pamba
Kilogramu 8.5 milioni
Nnje ya nchi
Bundaa oil industry
Mafuta ya Kupikia
Lita 2.7 million

Nnje ya nchi
S&C Ginning Co. Ltd.
Uchakataji Pamba
Kilogramu 8 million
Nnje ya nchi
Mafuta ya Kupikia
Lita 1.8 millioni
Ndani ya nchi
2
Tarime
Mara Coffee Ltd.
Kahawa Safi
Tani 942.3
Moshi na Soko la Kimataifa
Amir Hamza (T) Ltd

Kahawa Safi

Tani 77.6

Moshi na Soko la Kimataifa


ESSAB (T)
Kahawa Safi
Tani 174.8
Moshi na Soko la Kimataifa
3
Serengeti
Viwanda viwili (2) vya kutengeneza mafuta ya kupikia ya alizeti
Mafuta ya kupikia
Kiwanda kimoja kimefungwa na kingine hakijaanza kufanya kazi
Ndani ya nchi
4
Musoma
Prime Catch

Minofu ya Samaki

Kilogramu 20,200,451
Ulaya na
Kenya
Musoma processing
Minofu ya Samaki

Kilogramu 19,201,500
Ulaya na
Kenya
New Musoma textile
Nguo

Mita 102,120,201
Ndani ya nchi
Musoma Dairy
Processing Co
Maziwa

Lita 150,000

Kenya na
Musoma


Victoria milk
Maziwa
Lita 369,118
Mara
Winners co. ltd
Mikate
Pisi 1,220,101
Mara
Keki
Pisi 2,901,215
Bunda
Skonzi
Pisi 1,119,010
Mwanza
5
Rorya

Baraki Sisters Milk

Milk

-
Rorya,shirati na
Musoma
Riagoro
Soap
-
Rorya
Utegi
Animal skin
-
Rorya
Utegi

Spices

-

Ndani ya Nchi
Chanzo: Mara Region Investment Profile 2012

Hali ya uwekezaji katika Uchimbaji Madini
Madini ni miongoni mwa rasilimali zinazopatikana katika wilaya Rorya. Japokuwa bado hakuna Takwimu juu ya hali ya uchimbaji katika wilaya ya Rorya lakini kuna viashiria mbalimbali vya uwepo wa madini katika baadhi ya maeneo ya wilaya hii. Aidha kwa uopande mwingine utafiti wa awali inaonesha kwamba Gesi imeshagundulika katika maeneo ya Kogaja na Nyamusi. Kutokana na ugunduzi huu  inahitajika uwekezaji katika sekta mbalimbali za kijamii itakayoenda sambamba na ukuaji wa sekta ya madini. Kwa mfano Sekta ya madini inaenda sambamba na uboreshaji wa huduma za usafiri, mawasiliano, migahawa na mahoteli. Kwahiyo hizi zote ni fursa inayohitaji uwekezaji tena wa haraka. Vilevile inahitajika makampuni yatakayowekeza katika uchimbaji mkubwa na yenye tija.


Hali ya uwekezaji katika Mali asili na Utalii

Sekta ya utalii ni moja ya sekta zinazopaisha mkoa wa Mara. Baadhi ya vivutio vikubwa vinavyopatikana katika Mkoa wa Mara ni pamoja na Mbuga maarufu ya Serengeti pamoja na Ghuba ya Speke (Wilaya ya Bunda). Hizi zote zinatoa fursa ya ujenzi wa mahoteli ya kitalii na biashara mbalimbali inayoendana na Sekta husika. Katika wilaya ya Rorya vitvutio vya utalii ni visiwa vya Ryamakabe na Bugambwa. Haya maeneo yanahitajika uwekezaji wa makampuni ya utalii na miundombinu za kitalii ikiwemo mahoteli, maduka na biashara zingine zinazoendana na utalii.

No comments:

Post a Comment