![]() |
Muanzilishi wa Blog Hii |
Baada ya kufanya utafiti katika Mkoa wa Mara hususan katika Wilaya ya Rorya ameweza kugundua kuna Fursa na Rasilimali nyingi. Lakini licha uwepo wa fursa hizi maendeleo ya Rorya na wanarorya wenyewe haiendani na rasilimali zilizopo. Rasilimali hizo ni pamoja na Mali Asili, kama vile madini, Ardhi yenye Rutuba, Hali ya hewa nzuri na Rasilimali watu. Wilaya ya Rorya ina Vijana Wenye Nguvu ya kufanya kazi, Wasomi wengi, Wanasiasa wenye ushawishi mkubwa na ambao wameshawai kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nnje ya Serikali. Lakini ya cha ya haya yote bado maendeleo ni ya chini sana. Kwanini???
Muanzilishi wa blog hii katika utafiti wake ameweza kugundua kuwa licha ya uwepo wa rasilimali bado kuna kitu muhimu kinakosekana nayo ni "KIUNGANISHI". Mnaweza mkawa na rasilimali nyingi sana, wasomi wengi sana na nguvu kazi kubwa sana lakini endapo itakosekana Kitu cha kuunganisha hivi vitu vyote bado hautaweza kufanya kitu.
Lengo la blog hii ni Kuunganisha Wasomi na wadau wengine wa maendeleo katika kutambua Fursa mbali mbali za ajira na uwekezaji ndani ya wilaya ya Rorya. Ndani ya blog hii utaweza kupata Habari, Matukio, Makala, Changamoto na Fursa Mbali mbali inayopatikana ndani Ya wilaya ya Rorya.
"Kwa pamoja Maendeleo ya Rorya inawezekana"
No comments:
Post a Comment