Wilaya ya Rorya
Rorya ni wilaya mpya katika mkoa wa Mara. Hadi 2006 ilikuwa
sehemu ya magharibi ya wilaya ya Tarime. Mnamo mwaka 2007 iligawanywa kuwa
wilaya. Makao Makuu ya Wilaya ya Rorya ni Ingri Juu huku mji mkubwa katika
wilaya hii ni Shirati.
Wakazi walio wengi wa wilaya ya Rorya ni Wajaluo. Wakazi wengine wa eneo
hili ni Wakurya, Wakine, Wasimbiti na Wasuba
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya hii ilikuwa na wakazi
wapatao 265,241 waishio humo.
Jogorafia ya Rorya
Rorya ipo
Kaskazini mwa Tanzania ipo kati ya latitudo 1°00" – 1°45" kusini mwa
mstari wa Ikweta na longitudo 33° 30" – 35° 0" upande wa mashariki ya mstari wa Meridian.
Eneo la wilaya ya Rorya liko kati ya ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi
na Tarime upandwe wa mashariki. Upande wa kaskazini inapakana na Nchi ya Kenya
na upande wa kusini wilaya ya Musoma.
Wilaya hii
inakadiriwa kuwa na altitudo 800mm-1200mm kutoka usawa wa bahari na jotoridi la
eneo hili pia inakadiriwa kuwa ni kati ya 21-29 digrii sentigredi. Wastani wa
mvua kwa mwaka inakadiriwa kuwa kati ya 700mm hadi 1200mm.
Majimbo ya uchaguzi,
Tarafa na Kata
Mfumo
wa Tanzania wa uchaguzi imegawa nchi katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi.
Tangu mwaka uchaguzi wa mwaka 1995 wilaya ya Rorya ina jimbo moja ya uchaguzi
(Jimbo la Rorya). AidhaWilaya
ya rorya ina Tarafa nne nazo ni;
1.
Girango,
2.
Nyancha,
3.
Luo-Imbo
4.
Suba
5.
Rabuor
Vilevile wilaya hii hadi kufikia mwaka 2012 ilikuwa na
kata 21 nazo ni; (jumla ya wakazi mbele ya kata)
1. Bukura - 15,228
2. Bukwe - 9,920
3. Goribe - 9,915
4. Ikoma - 10,397
5. Kigunga - 13,824
6. Kirogo - 7,250
7. Kisumwa - 12,447
8. Kitembe - 9,845
9. Komuge - 13,651
10. Koryo - 7,652
11. Kyang'ombe- 18,438
12. Mirare - 12,416
13. Mkoma - 17,132
14. Nyahongo - 18,454
15. Nyamagaro - 17,006
16. Nyamtinga - 11,203
17. Nyamunga - 13,161
18. Nyathorogo- 14,809
19. Rabour - 11,259
20. Roche - 8,728
21. Tai - 12,506
Uchumi
Uchumi wa Rorya
ina shikiliwa na kilimo ambapo inakadiriwa takribani asilimia 89 ya wakazi wa
Wilaya ya Rorya wanategemea kilimo. Eneo la wilaya ya hii ina ukubwa wa heraki
291,375 inayofaa kwa kilimo lakini ni hekari
130,481 pekee ndio inayolimwa mpaka sasa. Vilevile eneo lenye ubwa wa
kilometa za mraba takriban 17350 inafaa kwa kilimo cha umwagiliaji kalini ni
kilometa za mraba 1,039 pekee ndio kilimo cha umwagiliaji inafanyika. Kilimo
katika wilaya ya Rorya kwa kiasi kikubwa inategemea jembe la mkono pamoja na ya
kukokota na Ng’ombe. Hii hupelekea shuguli ya kilimo kuwa na tija ndogo. Aidha
kilimo cha kisasa kinafanyika lakini na watu wachache. Mazao yanayolimwa katika
wilaya hii ni pamoja na Mihogo, Mahindi, Viazi vitamu, Mtama, maharage,
mbogamboga na matunda kwa kiasi kidogo. Shughuli zingine za kiuchumi katika
wilaya hii ni pamoja na yafuatayo;
Ufugaji
Zaidi ya 70% ya
wakazi wa Rorya hujihusisha na ufugaji (Ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku n.k).
Ufugaji husaidia wakazi wa Rorya kwa kuwapatia Chakula (Nyama, maziwa, mayai
n.k) pamoja na Kipato. Vile vile Mifugo hususan Ng’ombe na punda ni nyenzo
inayotumika na wakazi hawa kwa ajili ya kilimo. Asilimia kubwa ya ufugaji
katika eneo hili ni ufugaji wa asili jambo inayopelekea kuwa shughuli yenye
tija ndogo kwa wakazi hawa.
Viwanda
Wilaya ya Rorya
viwanda vidogovidogo ikiwemo Kiwanda cha
kutegeneza Sabuni, Kiwanda cha kuchakata Ngozi pamoja na kiwanda cha Maziwa.
Kwa kiasi fulani uwepo wa viwanda hivi vimesaidia kutoa ajira kwa wakazi wa
eneo hili lakini bado havijawa na tija kubwa kwa wakazi hawa.
Biashara
Vilevile wakazi wa
Rorya hujihusisha na na biashara mbalimbali kuanzia kubwa, kati pamoja na
biashara ndogondogo. Biashara inayofanyika ni pamoja na biashara ya mazao na
vyakula vya aina mbalimbali ikiwemo samaki, dagaa, mbogamboga na matunda n.k.
Vituo maarufu vya biashara katika wilaya hii ni pamoja na, Shirati, Utegi,
Ochuna, Randa na Mthana.
Madini
Mdini ni
rasilimali nyingine inayopatikana katika eneo hili japo uchimbaji mkubwa bado
haijaanza lakini kuna uchimbaji mdogomdogo inaendelea katika maeneo mbalimbali.
Japo bado hakuna takwimu juu ya hali ya uchimbaji na kipato itokanayo na madini
katika eneo hili lakini inasaidia kuwapatia wakazi wa eneo hili kipato.
Vilevile katika eneo hili kuna uchimbaji wa mawe, kokoto na michanga kwa jili
ya ujenzi.
Uvuvi
Wilaya ya Rorya
ina eneo inayofaa kwa uvuvi lenye ukubwa wa kilometa za mraba 7,252 kandokando
ya ziwa Viktoria ambapo jumla ya vijiji 23 vimezunguka eneo hili. Wanavijiji
hawa hutegemea sana uvuvi katika kuendesha maisha yao ikiwemo kipato na
chakula. Aina ya samaki inayovuliwa ni pamoja na Sangara (Mbuta-Kijaluo), Sato (Ngege-Kijaluo),
Dagaa (Omena-Kijaluo).
Ufugaji wa Nyuki
Hii ni shughuli
changa katika eneo hili. Haijanea miongoni nmwa wakazi wa Rorya kama shughuli
ya kuingiza kipato. Ufugaji nyuki inafanyika kwa njia za asili jambo
inayopelekea kuwa na manufaa madogo kwa wakazi wa eneo hili. Kuna takriban
Vikundi 10 vya wajasiriamali katika
vijiji mbalimbali wanaojihusisha na shughuli hii. Vikundi hivi vina jumla ya
mizinga 400.
Maliasili (Misitu, milima na mito)
Wilaya ya Rorya
ina maliasili mbalimbali ikiwemo Misitu, milima pamoja na Mito. Misitu
inachukua eneo lenye ubwa wa kilometa za mraba takriban 1,534sawa na 30% ya
ukubwa wa eneo lote la Wilaya ya Rorya. Asilimia 18 ya misitu hii humilikiwa na
na jamii yenyewe, asilimia 12 na watu binafsi ijulikanayo kama Ngitiri. Misitu
hii hutumika na wakazi hawa kwa ajili ya ujenzi, dawa na nishati. Vilele wilaya
ya Rorya ina mito miwili mikubwa, Mto Mara na Mto Mori isiyokauka mwaka mzima.
Pia kuna milima mbalimbali ikiwemo Mlima Rorya.
Rorya ni kubwa lakini kwa idadi ya vituo maarufu kwa ajili ya biashara does not make sense. Hii inatakiwa iangaliwe kwa mapana ili kukuza uchumi wa Rorya na maendeleo yake kwa ujumla.
ReplyDeleteHivi viwanda 3 vipo hai kweli au ni historia?
ReplyDeleteNimeona madini kumbe mchanga
ReplyDeleteNi vema ulivyotaja viwanda lakini haviko hai inasikitisha sana
ReplyDeleteMtoa historia ya Rorya huyu sijui katumwa kumfurahisha nani!?Viwanda!?
ReplyDeleteNyamaguku pia Ni kituo kikubwa Cha biashara,bila kusahau mialo maarufu Kama vile kibui,ruhu na kinesi ambapo Kuna kivuko kikubwa kinachounganisha Rorya na musoma mjini.ingefaa serikali itafute muwekezaji wa kiwanda Cha maziwa kinesi maarufu Kama Farm.kwani limekuwapori linalosaidia kwa wizi wa mifugo na kufichwa humo.
ReplyDelete